Sunday , 4th May , 2025

Kutoka Konde Music Worldwide Ibraah ameambiwa alipe Tsh Bilioni 1 na boss wake pesa ambayo imemshinda anataka msaada wa kuchangiwa na mashabiki.

Picha ya Harmonize na Ibraah wakiimba pamoja

Ibraah anasema "Dah hili limenishinda narudi kwenu watanzania mzee Konde anataka nimlipe Bilioni 1, Mimi tangu nianze muziki sijawahi kuingiza hata robo ya Bilioni".

"Kwa itakayempendeza ukiwa na jero au buku nisaidieni sitaki kupishana na mzee Konde, hili suala la kulipa Bilioni 1 linaninyima usingizi. Hofu yangu kipaji changu kupoteza na sina kazi nyingine".