Wednesday , 30th Apr , 2025

Mkali wa chaka to chaka Best Naso yupo kwenye mazungumzo na BASATA kwa ajili ya kupewa ushuru kutoka kwa wasanii wanaofanya shows hizo mikoani.

Picha ya msanii Best Naso

"Nipo na walezi wangu BASATA na leo nakutana nao nimewaambia hilo suala tunaangalia taratibu za mimi kupewa ushuru".

"Machaka mengi ya Tanzania nimeyaanzisha mimi kwa asilimi 95, mpaka kumbi zimejengwa kwa sababu" - Best Naso kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

Pia anasema shows za chaka to chaka ni kufanyika tofauti watu wanavyozichukulia na msanii akizifanya anaonekana ni wa vijijini na vichakani.