Wednesday , 23rd Apr , 2025

Brazil ni miongoni mwa nchi ambazo zina idadi kubwa ya wafungwa Duniani, na hii ni kutokana na makundi ya kihalifu, uuzaji wa madawa ya kulevya na vurugu za hapa na pale.

 

Kwa mujibu wa Lucrecia Franco ripota wa CGTN kutokea Rio de Janeiro, anasema Kwa sasa, Brazil ina zaidi ya watu 830,000 walioko gerezani, na kiwango cha makosa kujirudia (recidivism) kikiwa zaidi ya asilimia 80.

Kwenye kupunguza idadi ya wafungwa na kukuza uelewa wao, mwaka 2012 wizara ya sheria nchini Brazil ilitambulisha sheria ambayo itampunguzia mfungwa takribani siku 4 za kukaa gerezani ikiwa tu atasoma kitabu kizima na kuandika alichoelewa kwenye kitabu hicho.

Inakuwa kwenye mfumo huu, mfungwa anapewa siku 21 hadi 30 za kusoma baada ya hapo siku 10 ya kuandika alichopata au kuelewa. Kwa mwaka mfungwa anaweza kuwasilisha machapisho 12 kwenye vitabu alivyosoma na kupunguziwa siku 48 za kukaa gerezani.

Picha: u/BrainOld9460