Saturday , 15th Mar , 2025

Mmiliki mwenza wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe amesema ataondoka kwenye klabu hiyo iwapo mashabiki watamvunjia heshima kama vile ilivyofanyiwa familia ya Glazer.

Sir Jim Ratcliffe - Mmiliki mwenza wa Manchester United

Sir Jim mwenye umri wa miaka 72 mwaka jana alitumia £1.3bn kununua asilimia 28.94% ya klabu hiyo, katika mkataba ambao ulipelekea kampuni yake Ineos kusimamia uendeshaji wa soka.

Usimamizi wa Sir Jim umepunguza zaidi ya wafanyakazi 200 katika klabu hiyo, na kupanda kwa bei za tiketi zaa kuingilia uwanjani katikati mwa msimu huku akitangaza mipango ya kujenga uwanja mpya wa £2bn wenye uwezo wa kubeba mashabiki 100,000.

Familia ya Glazer isiyopendwa na mashabiki wa United kwasasa iliinunua klabu hiyo mwaka 2005 kwa kiwango kikubwa cha fedha na kubeba mataji matano ya EPL na taji moja la Uefa.