Tuesday , 11th Mar , 2025

Klabu ya Al Ahly imeomba kuahirisha mechi yake dhidi ya mpinzani wake Zamalek katika Ligi Kuu ya Misri iliyopangwa kufanyika leo saa 4:30 Usiku.

Al Ahly Fc

Al Ahly katika taarifa yao waliyoichapisha mapema hii leo wametishia kujitoa kwenye Ligi ya Misri iwapo mechi yao dhidi ya Zamalek itachezeshwa na mwamuzi wa Misri ambapo anaamini waamuzi wa taifa hilo haasimamii haki na usawa katika ligi hiyo.              

Al Ahly wamesema hawatacheza mechi hiyo hadi Chama cha soka nchini humo watakapoleta waamuzi kutoka nje ya mipaka ya Misri, na kusisitiza kwamba haitacheza ligi hiyo  endapo matakwa yake ya kutaka waamuzi kutoka nje ya nchi hayatatekelezwa.

Al Ahly inashika nafasi ya 2 katika msimamo wa ligi kuu nchini Misri wakiwa na alama 39 tofauti ya alama 7 na Zamalek anayeshika nafasi ya 3