Friday , 28th Feb , 2025

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) usiku wa kuamkia leo Februari 28, 2025, kimezindua jukwaa la kidigitali la kuchangia fedha lililopewa jina la #ToneTone.

Uzinduzi wa Tone Tone

Uzinduzi huo umefanyika katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Mikocheni Dar es Salaam, ambapo viongozi wakuu na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walijitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo huku diaspora wakishiriki kidigitali.

Fedha hizo zinazokusanywa kupitia kampeni ya #ToneTone na #ToneNimo zinalenga kuendesha kampeni ya 'No reforms no election' inayosimamiwa na chama hicho baada ya mkutano mkuu uliofanyika Januari 21, 2025 kuazimia hilo.

Baada ya kukusanywa fedha hizo zitatumika kama gharama ya kuwafikia wananchi kupitia mikutano ya hadhara maeneo mbalimbali nchini hadi vijijini, ili kutoa elimu na kuwaelewesha maana ya vuguvugu hilo.

Kampeni hiyo itadumu kwa miezi sita na kila mwananchi anapaswa kuchangia fedha na malengo waliyojiwekea kwa kuanza ni kukusanya shilingi bilioni 1.