
Lamine Yamal - Winga wa Klabu ya Barcelona
Akizungumza katika mahojiano na chombo kimoja cha habari Yamal amesema;
“Mimi Kwenda Real Madrid? hilo halina nafasi kwangu, yaani haiwezekani, sitakwenda kuitumikia Real Madrid” Alijibu Lamine Yamal alipoulizwa na mwandishi wa habari kuwa endapo Real Madrid watatuma ofa yupo tayari kwenda kuvaa jezi jezi ya Los Blancos?
“Ukishinda 0-3 au 0-4 wanaweza kusema wanachotaka, lakini mwisho hawawezi kufanya lolote, wanaona unawafunga kwenye uwanja wao, wanaona hawaezi kukufikia kwa ubora uwanjani ndiyo wanakuja na ajenda kama hizi lakini kiukweli siwezi kwenda Madrid”
"Ikiwa waliniimba kwamba mimi ni mweusi na maneno mengine mengi ya ubaguzi , niwaambie tu hilo halinisumbui , na ninajivunia utambulisho wangu" Yamal