
Enzo Maresca - Kocha wa Chelsea
The Blues walipoteza 3-0 Uwanja wa AMEX dhidi ya Brighton kwa mara ya pili ndani ya siku sita Ijumaa usiku, huku wakishindwa kupiga shuti hata moja lililolenga lango.
Maresca aliomba radhi kutokana na mwenendo wa timu yake kuwa mbaya zaidi tangu kuwasili kwake ingawa mwanzoni timu hiyo ilifanya vizuri hadi kufika nafasi ya pili katika msimamo wa EPL.
Chelsea imepata ushindi mara mbili pekee kati ya mechi zao tisa za mwisho za ligi, pia ni miongoni mwa timu sita pekee zilizokusanya alama chache, huku nafasi ya Kocha Maresca inaripotiwa kuwa salama kwa mujibu wa ripoti kutoka England.