![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2025/02/14/web-ukraine.jpg?itok=EzsJtdmu×tamp=1739545589)
Hayo yanajiri wakati Rais Donald Trump akisema maafisa wa Marekani, Urusi na Ukraine watakutana mjini Munich lakini Moscow inasema hawatatuma ujumbe katika mkutano wa usalama.
Taarifa zinasema kwamba Moscow inaweza kukumbwa na vikwazo na hatua za kijeshi iwapo Vladimir Putin atashindwa kukubaliana na makubaliano ya amani yanayohakikisha uhuru wa muda mrefu wa Ukraine.
Washirika wa Nato wa Marekani bado wanaitikia tangazo la kushangaza la Trump kwamba yeye na Putin walikubaliana kwa njia ya simu kuanza mazungumzo ya kumaliza vita.
Rais Zelensky amesema makubaliano yoyote ya aina hiyo lazima yahusishe Ukraine
Ni karibu miaka mitatu tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake kamili wa Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky yeye tayari amewasili, na kutumia mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kusema mazungumzo yake hadi sasa na Trump hayatoshi kuunda mpango wa amani.
Zelensky anatarajiwa kukutana na Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance baadaye leo na pia amezungumza na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, ambaye alirejelea msaada wa nchi hiyo kwa Kyiv kwa muda mrefu kama inahitajika.