Monday , 3rd Feb , 2025

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Mbeshi Mliambelele mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa kijiji cha Mfinga, Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa, amefariki Dunia baada ya kushambuliwa na Tembo wanne.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo inatajwa kuwa mnamo majira ya saa Tatu asubuhi Tembo hao walifika kijijini hapo, wakaanza kuharibu mahindi shambani ndipo wananchi wakachukua jukumu la kuwafukuza kwa kuwapiga mawe, taratibu wakatokomea kwenye mahindi marefu zaidi.

Licha ya Tembo hao kwenda mbali lakini baadhi ya vijana waliendelea kuwafuata huku wakipiga kelele na kuwarushia mawe, baadae Tembo waliwageukia vijana hao na wakaanza kumshambulia kijana Mbeshi huku wenzake wakimkimbia bila msaada Wowote hatimaye akapoteza maisha.

Kwa upande wao maafisa wanyamapori na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukile wamefika eneo la tukio ambapo wametoa pole kwa familia na kuwataka wananchi kuchukua tahadhali mapema dhidi ya wanyama hao. Kijana Mbeshi ameacha Mtotomjane na mtoto mmoja. #EastAfricaTV