Wednesday , 22nd Jan , 2025

Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA limemthibitisha John Mnyika kuendelea kushika wadhifa wake wa ukatibu mkuu wa chama hicho.

Viongozi CHADEMA walioteuliwa

Katika mkutano wa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho uliofanyika jana jioni Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Tundu Lissu alimpendekeza John Mnyika kuendelea na wadhifa huo kwa kile alichokieleza kwamba Mnyika amekulia kwenye chama, ameshika dhamana kubwa ndani ya chama ni mmoja wa wafanyakazi waadilifu wa chama hicho.

Aidha Baraza Kuu la chama hicho limewathibitisha Godbless Lema, Dr. Rugemeleza  Nshala, Rose Mayemba, Salma Mussa Kasanzu na  Hafidh Ali Saleh kuwa wajumbe wa kamati kuu.

Katika uchaguzi wa ndani wa CHADEMA wa kumpata mwenyekiti, Tundu Lissu alishinda kinyang'anyiro hicho kwa kupata kura 513 (51.5%) akiwashinda wapinzani wake Freeman Mbowe aliyepata kura 482 (48.3%) na Odero Odero aliyepata kura moja.