Monday , 6th Jan , 2025

Timu ya Simba SC inaongoza msimamo wa ligi kuu Tanzania kwa tofauti ya alama 1 ikiwa na alama 40 ikifuatiwa na Yanga SC yenye alama 39. Kikosi hiko cha Wekundu wa Msimbazi kimekuwa hakichezi soka la kuvutia kama Mashabiki wengi wa Soka Tanzania wangependa kuona timu hiyo ikicheza.

Kocha Fadlu Davids yeye ndiye sababu ya timu yake kuongoza msimamo wa ligi msimu huu licha ya kuwa ndio msimu wake wa kwanza kwenye kikosi hiko huku kukiwa na presha kubwa ya kuhitaji kushinda ubingwa wa ligi sambamba na kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika kwa ngazi za Vilabu. Kocha huyo raia wa Afrika ya kusini ameijenga timu yake kupata matokeo chanya katika hali yoyote bila kuangalia inachezaje.

Timu ya Simba SC inaongoza msimamo wa ligi kuu Tanzania kwa tofauti ya alama 1 ikiwa na alama 40 ikifuatiwa na Yanga SC yenye alama 39. Kikosi hiko cha Wekundu wa Msimbazi kimekuwa hakichezi soka la kuvutia kama Mashabiki wengi wa Soka Tanzania wangependa kuona timu hiyo ikicheza kutokana na utamaduni wake.

Kocha Fadlu Davids yeye ndiye sababu ya timu yake kuongoza msimamo wa ligi msimu huu licha ya kuwa ndio msimu wake wa kwanza kwenye kikosi hiko huku kukiwa na presha kubwa ya kuhitaji kushinda ubingwa wa ligi sambamba na kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika kwa ngazi za Vilabu. Kocha huyo raia wa Afrika ya kusini ameijenga timu yake kupata matokeo chanya katika hali yoyote bila kuangalia inachezaje.

Objective Foootball ndio aina ya mpira kikosi cha Simba SC kinacheza yani mpira wa malengo na sim mpira wa kufurahisha wa pasi nyingi na burudani. Fadlu ameijenga timu yake kuwa mashine ya kupata matokeo ya alama tatu kwa kuweza kugawa aina mbili za uchezaji wa kikosi hiko. Simba inayocheza Dar es salaam au uwanja wake wa nyumbani ni tofauti na ile utakayokwenda kuiona ikicheza ugenini.

Michezo yote migumu ambayo kwenye makaratasi ilionekana ingeipa shida kikosi cha Mwalimu Fadlu tmu yake imeshinda kwa goli 1-0 hii inaonyesha jinsi gani ameijenga timu yake kwa kuangalia zaidi mbinu na si kuburudisha Mashabiki. Michezo miwili mfululizo ugenini yote ikitizamiwa kupoteza alama Simba imeondoka na alama 3 huku ikiwa hairuhusu nyavu zake kuguswa. Mchezo dhidi ya Singida Black Stars uliochezwa mkoani Singida ulimalizika kwa goli 1-0, mchezo wa siku ya jana shidi ya CS Sfaxien uliopigwa nchini Tunisia pia umemalizika  kwa goli 1-0.

Kocha mwenye heshima kubwa Duniani Sir Alex Ferguson aliwahi kukaririwa akisema safu bora ya ushambuliaji inaweza kukufanya kushinda mechi lakini safu imara ya ulinzi inaweza kukushindia ubingwa hii ndio sababu Mwalimu Fadlu anaangalia zaidi kutokuruhusu goli kwani malengo yake msimu huu ni kushinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara pamoja na kombe la shirikisho la CRDB.

Simba SC imeruhusu magoli 5 pekee katika michezo 15 ya ligi kuu ambayo imekwishacheza mpaka sasa huku ikiwa imefunga magoli 31 hii inakupa picha jinsi gani timu hiyo ilivyo imara kwenye maeneo yote muhimu uwanjani kufunga na kuzuia.

Kocha wa Simba SC Fadlu Davids anatoa fundisho kwa Makocha wengine Tanzania jinsi gani ya kucheza michezo ya nyumbani na ugenini ili kuweza kutimiza malengo ambayo wamewekewa na Maboss wa timu zao.Huwezi kucheza sawa ugenini na nyumbani unapokuwa nyumbani unaenda kwa kushanbulia huku ukiwa ugenini unapaswa  kucheza kwa tahadhari ili usipoteze mchezo ndicho anachokifanya Fadlu Davids aliyeleta tofauti kubwa kwenye kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.