Wednesday , 18th Dec , 2024

Linapofika suala la kumiliki chombo cha usafiri kama vile gari wengi utasikia wakitaja majina makubwa na yaliyozoeleka kwa wengi ni mara chache sana mtu kuchagua aina ya gari kutoka kwenye kampuni ambayo haifahamiki.

 

Sasa kuna baadhi ya majina makubwa kwenye makampuni ya magari ambayo yanamilikiwa na makampuni mengine, pengini ulikuwa unafahamu au ndiyo utafahamu hapa kwa mara ya kwanza.

Mwaka 1989 Ford na Jaguar waliungana na kutengeneza kampuni moja, 1994 BMW na Rover Group waliungana kutengeneza kampuni moja ambayo baadae ilikuja kununuliwa na kampuni ya Tata,  Nissan na Mitsubishi Motors waliungana wakatengeneza kampuni moja, Porsche na Volkswagen waliungana wakatengeneza kampuni moja.

Miongoni mwa sababu ambazo zinatajwa kama sababu ya kampuni hizi kuungana ni kuzalisha bidhaa bora zaidi, sababu ya kiuchumi, kuliteka soko katika namna mpya, kampuni kuuzwa.

Ukiachana na zote hizo, habari mpya mjini kuelekea mwaka 2025 ni kwamba kampuni ya Nissan na Honda wako kwenye mazungumzo ya kuunganisha kampuni hizo ili kutengeneza kampuni moja kubwa ambayo itakuwa rahisi kwao kupambana na washindani wao kama vile Toyota na Volkswagen.