Monday , 2nd Dec , 2024

Jeshi la Polisi Tanzania limethibitisha kuwa Kiongozi wa Ngome ya Vijana wa ACT - Wazalendo Abdul Nondo amepatikana baada ya kutelekezwa eneo la Fukwe za Coco Kinondoni Jijini Dar es salaam

Taarifa ya Polisi imesema kuwa Nondo baada ya kutelekezwa na watu asiowajua katika eneo hilo alisimamisha Bodaboda na kumuelekeza amfikishe katika Ofisi za Chama chake Magomeni Jijini Dar es salaam ambapo alifikishwa hapo saa tano usiku na kuonana na viongozi wake kabla ya kupelekwa

Hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake

Taarifa za kutekwa kwa Nondo zilitolewa na Chama chake Jana jumapili na baadae Polisi walithibitisha kuwa wanamtafuta kiongozi huyo baada ya kuchukuliwa eneo la Stendi Mbezi Jijini Dar es salaam

Polisi wamesema wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo