Thursday , 28th Nov , 2024

Klabu ya Simba  siku ya jana ilipata ushindi wake wa kwanza wa katika kombe la shirikisho mchezo wa kwanza kundi A dhidi ya FC Bravos Do Maquis kutoka nchini Angola. Goli la Jean Charles Ahoua lilitosha kuipa alama 3 muhimu klabu yake mchezo uliopigwa uwanja Benjamini Mkapa Dar es salaam.

Fadlu Davies anapaswa kubadilika kwenye hili hakuna anayehoji sababu Simba inaondoka na matokeo ya ushindi ila ikatokea inaanza kudondosha alama huku akiwa anaendelea kufanya mzunguko wa kikosi chake atajikuta matatani kwani Mashabiki wataanza kuhoji na presha ikishakuwa kubwa hupelekea viongozi kuchukua hatua ya kumfuta kazi Mwalimu. Timu zote zinazochukua ubingwa huwa zinavikosi vya kwanza walau kwa asilimia 75 mpaka 80 ya Wachezaji walewale kucheza pamoja kwa muda mrefu.

Sawa kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kimefanikiwa kuondoka na ushindi ila kuna kitu bado hakipo sawa kiuchezaji mpaka upangaji wa timu kwa Mwalimu Fadlu Davies. Timu yake inakosa uwiano wa Wachezaji ambao wanacheza kwa pamoja mfululizo kwenye michezo ya mashindano mbalimbali inayoshiriki. Kuna baadhi  ya maeneo Wachezaji wamekuwa wakibadilishwa kila mechi hii inaweza kuleta athari pindi Simba itakapocheza na timu pinzani ambayo inacheza kitimu na iliyozoeana kwa muda mrefu.

Umoja wa kiuchezaji ndani ya uwanja au muunganiko wa kiuchezaji hauji kwa kubadili kikosi mara kwa mara bali kwa kuamini kwenye Wachezaji ambao wanaweza kumpatia uwiano sahihi wa kushambulia na kuzuia ili iweze kucheza kwa uhusiano mzuri ndani ya uwanja kwa vile Wachezaji wamecheza kwa pamoja michezo mingi.

Eneo ambalo klabu ya Simba huwa halibadilishwi na Mwalimu Fadlu ni safu yake ya Ulinzi kuanzia golini endapo Golikipa wake namba moja anapokuwa yuko fiti.Golini huwa anaanza Moussa Camarra,Beki wa kulia Shomari Kapombe, Beki wa kushoto Mohamed Hussein Zimbwe Junior Mabeki wa kati Che Malone Fondo na Abdulrazak Hamza kuanzia sehemu ya kiungo cha kukaba kuwekuwa kunafanyika mabadiliko ya  mara kwa mara.

Hii inamaana gani kiuchezaji? inamaanisha kuna kipindi timu inakosa uwiano wa kimaelewano kiuchezaji kuanzia safu ya kiungo yaani kukatika na kumezwa na Wapinzani. Mechi zote timu ya Simba iliyocheza msimu huu inacheza vizuri dakika 45 ya kipindi cha kwanza kipindi cha pili timu huwa inapoteza ubora wake na uwiano kiuchezaji na kusababisha wapinzani kuishambulia sana.

Ni vizuri kufanya mzunguko wa Wachezaji ili kila mmoja apate muda wa kucheza na kuisaidia timu kufikia malengo,lakini kuna muda inapswa kuwa na kikosi cha kwanza kinachofahamika ambacho kitaweza kuisgi kwenye misingi ya falsafa za Mwalimu, chapili ili timu icheze kitimu inapaswa kuwepo na kikosi cha kwanza ambacho kinacheza kwa pamoja muda mrefu hii hujenga kuaminiana kwa Wachezaji ndani ya uwanja kwa vile kila mmoja atakuwa anafahamu nguvu na mapungufu mwenzake au aina gani ya pasi anapaswa kupigiwa ili alete madhara kwa mpinzani.

Mechi nne za hivi karibuni kikosi cha Mwalimu Fadlu kimemaliza kwa ushindi wa goli 1-0 katika mechi tatu hii ni nzuri, kwa vile timu inaonekana imeimarika kiulinzi swali la kujiuliza je ni nafasi ngapi za kufunga timu hiyo inatengeza ndani ya dakika 90 za kila mchezo? jibu lake ni rahisi ni nafasi chache je hii inasababishwa na nini? Wachezaji wa sehemu ya kiungo cha kushambulia kutokutengeneza nafasi za kutosha kwa washambuliaji. Hili haliji kwa bahati mbaya kuna sehemu Wachezaji wanapoteza kuelewana kutokana na kutokucheza kwa pamoja kwenye idadi kubwa ya michezo.

Fadlu Davies anapaswa kubadilika kwenye hili hakuna anayehoji sababu Simba inaondoka na matokeo ya ushindi ila ikatokea inaanza kudondosha alama huku akiwa anaendelea kufanya mzunguko wa kikosi chake atajikuta matatani kwani Mashabiki wataanza kuhoji na presha ikishakuwa kubwa hupelekea viongozi kuchukua hatua ya kumfuta kazi Mwalimu. Timu zote zinazochukua ubingwa huwa zinavikosi vya kwanza walau kwa asilimia 75 mpaka 80 ya Wachezaji walewale kucheza pamoja kwa muda mrefu.

Tunafahamu timu hiyo inaendelea kujijenga huku ikiwa mashindanoni Mwalimu Mwalimu anapaswa kutengeneza taswira ya kikosi chake cha kwanza ambacho kinaweza kucheza kwa muda mrefu ili falsafa yake iweze kueleweka na kuleta faida kwa timu yake.