Tuesday , 19th Nov , 2024

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeahidi kutojitoa kwenye mchakato mzima na ushiriki wa Uchaguzi wa Serikali kama ilivyotokea miaka ya nyuma ili waweze kupata viongozi watakaowawakilisha kwenye ngazi ya jamii.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati anaongea na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho mikocheni jijini Dar es Salaam.
"Yaani Chama cha Mapinduzi (CCM) hawaoni aibu kupambana na vyama vya upinzani ambavyo havina fedha, havina vitendea kazi, havina magari, watu wanajitolea lakini wao wanalipwa kwa kodi zeti bado wanaweza kuasimama eti wanajiweza wakajigamba eti
wamepita kwa asilimia miabmoja wakati Dunia nzima inaona
wakiengua watu wetu, haya mambo yanaaudhi wanaolia ni wengi, na wengi wanalia wanasem Mwenyekiti (Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa) tujitoe kwenye uchaguzi (wa
serikali za mitaa 2024), wengine wanalia wanaseama tutapambana mpaka hatua ya mwishio, sisi (CHADEMA) Kamati Kuu yetu tulikaa kikao cha Kamati Kuu Mtwara tarehe 06/03/2024 na likatoka azimio la Kamati Kuu ambalo tulilitoa kwamba tushiriki uchaguzi huu" Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA.

Kuhusu migogoro ndani ya Chama hicho Mbowe anatolea ufafanuzi.

"Kuna wakati tunateleza, Mbowe anaweza akateleza, Makamu anaweza akateleza kauli, Katibu Mkuu anaweza akateleza kauli
lakini kwamba tuna mnyukano?, tumejenga hiki chama (CHADEMA) kwa maumivu makubwa, na sisi wote tumeshaapa tutakilinda chama hiki kwa gharama yoyote ile kwa hiyo kama kuna mtu anafikiria eti kuna mgogoro CHADEMA ambao utakigawa chama, tuko wamoja watu watanyukana tu" Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA.

Aidha Mbowe anasema wamejiandaa kurudisha chama hicho kileleni kama kilivyokuwa miaka ya nyuma.
"Kama chama hiki (Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA) tulifika kilele chetu kwenye uchaguzi wa
mwaka 2015, itakumbukwa kuwa wakati huo chama hiki kilishafika hatua ya kuwa na Wabunge 72 kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna chamam chochote nchi hii kilishafikisha idadi hiyo ya Wabunge, kwa sababu ya jasho na damu na maumivu ambayo tumeyapitia wote huku kila mmoja akiwa na mchango wake", Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA.