Monday , 18th Nov , 2024

Aliyekuwa Kocha mkuu wa timu ya KMC FC ya Dar es salaam Abdihamid Moalin ametangazwa na klabu ya Yanga kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo leo mchana.Utambulisho huo umemaliza yale mazungumzo ya chinichini kuhusiana na wapi atafanya kazi Kocha huyo baada ya kuondoka KMC FC.

Nafasi ya Ukurugenzi wa ufundi ni nafasi nyeti sana kwenye timu kwani mipango ya timu kuanzia falsafa ya timu aina ya uchezaji wa timu Wachezaji wanaohitajika na timu kulingana na aina ya falsafa iliyopo kwa wakati huo, mipango ya baadae aina gani ya Kocha aajiriwe yote ipo chini ya utendaji wa Mkurugenzi wa ufundi.

Aliyekuwa Kocha mkuu wa timu ya KMC FC ya Dar es salaam Abdihamid Moalin ametangazwa na klabu ya Yanga kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo leo mchana.Utambulisho huo umemaliza yale mazungumzo ya chinichini kuhusiana na wapi atafanya kazi Kocha huyo baada ya kuondoka timu ya KMC.

Moalin raia wa Marekani mwenye asili ya Somalia anauzoefu na mpira wa Tanzania baada ya kuhudumu kwenye timu za Azam FC na KMC FC akiwa Kocha mkuu wa vilabu hivyo vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara.

Cheo cha Ukurugenzi wa ufundi ni kipya kwenye mpira wetu wa Tanzania Yanga SC iliwahi kumuweka Hans Van Pluijm kwenye nafasi hiyo kipindi ambacho George Lwandamina akiwa Kocha wa kikosi cha Wanachi huku Yusuf Manji alikuwa Mfadhiri wa kikosi hiko.

Nafasi ya Ukurugenzi wa ufundi ni nafasi nyeti sana kwenye timu kwani mipango ya timu kuanzia falsafa ya timu aina ya uchezaji wa timu Wachezaji wanaohitajika na timu kulingana na aina ya falsafa iliyopo kwa wakati huo, mipango ya baadae aina gani ya Kocha aajiriwe yote ipo chini ya utendaji wa Mkurugenzi wa ufundi.

Kazi ya kwanza ya Moalin kwenye ajira yake mpya itakuwa kuhakikisha Wachezaji wa Yanga SC wanarudisha viwango vyao ili kutetea ubingwa wake wa ligi kuu Tanzania bara kombe la shirikisho Tanzania pamoja na kufanya vizuri michuano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu Afrika.

Klabu hiyo bingwa wa kihistoria ligi kuu Tanzania bara imemfukuza aliyekuwa Kocha wake mkuu Muargentina Miguel Gamondi nafasi yake imechukuliwa na Sead Ramovic raia wa Ujerumani ili kuhakikisha Yanga SC inatimiza malengo yake ya msimu huu.

Kazi yake kubwa ya pili itakuwa kuhakikisha anaiandaa mipango ya muda mrefu wa kikosi cha Wanajangwani kuanzia kwenye kikosi cha Vijana na aina ya Wachezaji wenye umri mdogo wanaopaswa  kusajiliwa ili kuifanya timu hiyo kutawala ligi kwa muda mrefu huku ikihakikisha inafanya biashara kuingiza pesa kwa kuuza Wachezaji.

Wasiwasi wangu utabaki eneo la weledi la viongozi wa timu zetu za vilabu Tanzania kama maamuzi atakayokuwa anafanya kwenye kazi yake yatatokana na yeye mwenyewe ama kuna Watu watakaokuwa wanamfanyia hayo maamuzi kwa niaba yake? Je mawazo yake yataheshimika klabuni humo ama atakuwa Mkurugenzi wa ufundi jina huku maamuzi yakifanywa na wengine? muda utakuwa shahidi mzuri wa kunijibu maswali yangu.