Monday , 11th Nov , 2024

Zikiwa zimechezwa raundi 12 za Ligi kuu soka nchini Italia Serie A, mbio za ubingwa zinaonekana kuwa ngumu kwenye michezo hii ya awali ya Ligi. Ambapo timu inayoongoza Ligi ni Napoli wanatofautiana alama mbili tu na Juventus wanaoshika nafasi ya sita kwenye msimamo.

Msimamo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A baada ya michezo 12 kuchezwa.

Tukiwa tunaeleka kwenye mapumziko ya kupisha kalenda ya kimataifa ya FIFA (FIFA international break) Napoli wanaongoza Ligi wakiwa na alama 26 tofauti ya alama 1 dhidi ya timu 4 zinazofuata kwenye msimamo ambazo ni Atalanta, Fiorentina, Inter Milan na Lazio zote zina alama sawa 25. Na juventus wapo nafasi ya 6 wakiwa na alama 24.

Inter Milan ndio mabingwa watetezi wanakibarua cha kuutetea ubingwa, wapo nafasi ya 4 wakiwa na alama 25, na katika michezo 12 waliyocheza wameshinda michezo 7 sare michezo 4 na wamefungwa mchezo 1.

Swali ni nani atakuwa bingwa wa Ligi Kuu Italia msimu huu 2024-25?