Monday , 11th Nov , 2024

Klabu ya Liverpool imepewa asilimia 59.3% kuwa mabingwa wa Ligi kuu soka nchini Uingereza EPL baada ya kushinda michezo 9 kati ya 11 iliyochezwa mpaka sasa. Majogoo ndio vinara wa Ligi wanaongoza kwa tofauti ya alama 5 dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City.

Kikosi cha Liverpool msimu 2024-25 kinapewa nafasi ya kuwa mabingwa wa Ligi kuu Uingereza EPL msimu huu.

Liverpool wanaongoza Ligi wakiwa na alama 28 tofauti ya alama 5 dhidi ya Man city wenye alama 23, tofauti hii ni baada ya Manchester City kupoteza mchezo wa pili mfululizo wa Ligi kuu kwa kufungwa na Brighton mabao 2-1 ambao mchezo wa pili mfululizo wa Ligi Kuu wanafungwa.

 

Kwa mujibu wa Super Compture ya Opta taasisi inayohusika na ukusanyaji wa takwimu za mshezo wa soka, mwanzoni mwa msimu Liverpool ilipewa asilimia 5% ya kuwa mabingwa wa EPL msimu huu wakati Manchester City walipewa asilimia 82%. Lakini baada ya raundi 11 za EPL kuchezwa sasa Liverpool ndio wanapigiwa chapuo kuwa mabingwa wa EPL msimu huu 2024-25 wamepewa asilimia 59.3 za kutwaa kombe.