Friday , 8th Nov , 2024

Mshambuliaji wa timu ya Singida Black Stars Marouf Tchakei,amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2024/25, huku Rachid Taoussi wa Azam FC akichaguliwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.

Tchakei alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo kwa mwezi Oktoba akiwashinda Lusajo Mwaikenda wa Azam FC na Pacome Zouzoua wa Yanga, alioingia nao fainali katika mchakato wa tuzo za mwezi uliofanywa na Kamati ya tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa upande wa Taoussi aliyeingia fainali katika mchakato huo na Abdulhamid Moallin wa KMC na Denis Kitambi wa Singida Black Stars,aliiongoza Azam FC kushinda michezo yote mitatu iliyocheza na kupanda kwa nafasi moja kutoka ya tano hadi ya nne. Azam ilizifunga Namungo bao 1-0, Tanzania Prisons mabao 2-0 na Ken Gold mabao 4-1.

Marouf Tchakei raia wa Togo amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu kwa kuchangia mazuri yote yanayofanywa na kikosi cha Singida Black Stars mwezi Oktoba ameisaidia Singida kushinda michezo mitatu na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Dar es salaam Young Africans ambao kikosi hiko kilipoteza kwa goli 1-0.

Rachid Taoussi amebadili vitu vingi klabu ya Azam kwa kuhakikisha timu inashinda huku akiwa anajenga kikosi chake, raia huyo wa Morocco hakufanikiwa kuanza na timu hiyo Matajiri wa kutoka Chamazi Mbagala Dar es salaam aliikuta timu imesajiliwa na kuanza msimu wa ligi kwa kazi aliyoifanya mwezi Oktoba imempa tuzo ya Kocha bora wa mwezi.

Ligi imesimama kupisha ratiba ya michezo ya kimataifa kwa timu za taifa kufuzu AFCON2025 baada ya michezo ya timu za taifa kutakuwa na michezo ya klabu bingwa pamoja na shirikisho Afrika ligi kuu itarejea tarehe 21 Novemba.