Tuesday , 5th Nov , 2024

Jinamizi la majeruhi limeendelea kumuandama Nahodha wa timu ya Brazil Neymar Junior baada ya jana kuumia tena misuli kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa barani Asia uliozikutanisha timu za Al-Hilal dhidi ya Esteghlal jana Jumatatu Novemba 4, 2024.

Nyota huyo wa zamani wa Santos ya Brazil amekitumikia kikosi cha Al-Hilal michezo saba tu tangu ajiunge na timu hiyo kutokea PSG mwaka 2023.

Jinamizi la majeruhi limeendelea kumuandama Nahodha wa timu ya Brazil Neymar Junior baada ya jana kuumia tena misuli kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa barani Asia uliozikutanisha timu za Al-Hilal dhidi ya Esteghlal jana Jumatatu Novemba 4, 2024.

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona FC na PSG ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 32 alikaa nje bila kucheza zaidi ya miezi 12 akiuguza goti lake na sasa amepata majeraha mapya ya misuli,bado hakuna taarifa rasmi za Daktari kutoka ndani ya timu hiyo zinazoelezea muda ambao atakaa tena nje ya uwanja.

Neymar amesema ni kawaida Madaktari wameshamtahadharisha kwamba atakutana na kitu kama hiko alichokutana nacho kupata maumivu ya misuli na nyama za paja kutokana na kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu hivyo atakuwa sawa akiendelea kucheza mara kwa mara.

Nyota huyo wa zamani wa Santos ya Brazil amekutumia kikosi cha Al-Hilal michezo saba tu tangu ajiunge na timu hiyo kutokea PSG mwaka 2023.

Neymar alipata jeraha kubwa la goti Oktoba 2023 kwenye mchezo wa kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Uruguay lililomsababishia kukaa nje kwa muda mrefu bila kucheza michezo ya kiushindani.

Hilo ni pengo jipya kwa Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Dorival Júnior katika harakati za kikosi hiko kufuzu fainali za kombe la Dunia mwaka 2026 zitakazofanyika nchi tatu za Marekani, Canada na Mexico.Timu hiyo  Mabingwa wa kihistoria wa kombe la Dunia inashika nafasi ya 4 ukanda wa CONBOL michauno ya kufuzu fainali hizo ikiwa imekusanya alama 16 baada ya kucheza michezo 10.

Michezo miwili ijayo ya kikosi cha Mwalimu  Dorival itakuwa dhidi ya Venezuela na Uruguay Neymar angekuwa ongezeko muhimu kwa taifa lake kukosekana kwake kunafanya michezo ya timu hiyo kuwa migumu kutokana na kumkosa Mchezaji mwenye uwezo wa kuzifungua safu za ulinzi za timu Pinzani pamoja na kufunga.