Muda mrefu Tanzania tumekuwa kwenye kilio kupata waamuzi wenye ubora wa kuchezesha michuano mikubwa ya CAF. Sasa tumeanza kuona mwanga tunapaswa kuongeza juhudi ya kuandaa Waamuzi ambao watakuwa na ubora mkubwa kuanzia kwenye ligi yetu ya ndani ambao watatuletea heshima taifa letu.
Waamuzi wa Tanzania Ahmed Arajiga, Frank Komba, Hamdani Said na Elly Sasii wameteuliwa na CAF kuwa Waamuzi watakaochezesha mchezo wa Kufuzu AFCON 2025, Cameroon vs Zimbabwe utakaochezwa Novemba 19,2024.
Muda mrefu Tanzania tumekuwa kwenye kilio kupata waamuzi wenye ubora wa kuchezesha michuano mikubwa ya CAF.Tumeanza kuona mwanga tunapaswa kuongeza juhudi ya kuandaa Waamuzi ambao watakuwa na ubora mkubwa kuanzia kwenye ligi yetu ya ndani ambao watatuletea heshima taifa letu.
Waamuzi wengi wanaochezesha ligi kuu Tanzania bara wanamatatizo ya kutafasiri sheria kumi na saba za mchezo wa mpira wa miguu, kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa Wadau wa soka nchini kuhusiana na ubora wa Marefarii ambao tunawazalisha.
Ubora wa ligi yetu uendane na wale ambao wanaohusika kwenye kuifanikisha ligi yetu kuanzia Shirikisho la mpira kutengeneza mipango mizuri na inayotekelezeka ya maendeleo ya soka kuanzia kwenye kuzalisha Wachezaji, Wakufunzi na Waamuzi ili tupate ubora unaostahiki kwenye mpira wetu kuendana na uwekezaji unaoendelea kufanyika kwenye sekta ya michezo nchini.
Ligi ya Tanzania ni miongoni mwa ligi bora tano barani Afrika kwa taswira hivyo tunapaswa kuongeza uwekezaji ili ligi yetu ifikie ubora wa ligi za Afrika ya Kaskazini.Fedha inapaswa kutumika , kwenye ujenzi wa miundombinu ambayo itafanya mpira kuchezwa kila sehemu nchini ili kuamsha hamasa kwa Vijana kujiingiza kwenye nafasi mbalimbali za sektaya michezo.
Arajiga anasifiwa na Wadau wengi wa soka Tanzania ndiye Refarii pekee ambaye ana ubora wa kuchezesha kwenye michezo mikubwa ya ligi yetu, uwepo wake pekee hautoshi tunapaswa kuzalisha kina Arajiga wengi ili inapofikia kutoa waamuzi wa kuchezesha mashindano makubwa ya CAF na FIFA na sisi tujivunie kwa kutoa Waamuzi ambao watapeperusha vizuri bendera ya Tanzania kwenye mpira wa kimataifa.