Thursday , 24th Oct , 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amewataka waumini wa Kijiji cha  Ikuyu kilichopo katika  Tarafa ya Kibakwe Wilayani Mpwapwa kuwa mstari wa mbele katika kujitolea fedha na vitu mbalimbali ili kutatua changamoto mbalimbali

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene

zinazoyakabili makanisa badala ya kutegemea misaada kutoka kwa viongozi.

Waziri Simbachawene ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na waumini na viongozi wa madhehebu mbalimbali walioshiriki katika  Mkutano wa Umoja wa Makanisa Ikuyu uliofanyika katika Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT).

Amesema kipato cha wananchi wa Kijiji cha Ikuyu ni kikubwa kulingana na na shughuli mbalimbali za kiuchumi wanazoziendesha ikiwemo kilimo cha kibiashara cha vitunguu na mahindi lakini majitoleo yao katika kazi ya Mungu yamekuwa sio wa kuridhisha.

Amesema hali ya majengo ya makanisa yaliyopo katika eneo hilo ni machakavu kutokana na waumini kutokuwa na utamaduni kwa kujitoa katika kazi ya Mungu.

"Nimesilikiliza risala yenu  mmeniomba nichangie zaidi ya Sh. Milioni 25 kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoyakabili makanisa yenu, nataka niwaambie ni lazima kila mmoja wetu ajitoe ili kufanikisha hili kwa pekee yangu nitachangia pale nitakapoweza," amesema Mhe. Simbachawene.