Taarifa hiyo iliyotolewa na jeshi la polisi imeeleza jeshi la polisi linawashikilia madereva hao wa basi la kampuni hiyo kwa kuendesha basi kizembe na kusababisha ajali ambapo uchunguzi unaendelea na pindi uchunguzi utakapo kamilika watapandishwa mahakamani
Jeshi la polisi limeendelea kutoa wito kwa madereva wote wanaoendesha vyombo vya moto kuendesha kwa kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara zinazoepikika.