Akiongea na EATV, katibu mtendaji wa Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini LATRA CCC, anaelezea maeneo ambayo wanaona yanahitaji kuongezewa nguvu.
"Ni kuhusu usalama wao wa kusafiri uksiema watu wenye ulemavu, ukisema watu wenye uhitaji maalum, wajawazito kwa maana wote wanahitaji kupata huduima nzuri, kwahiyo kwa kuanzia tuliona hili gap uhitaji mkubwa sana katika swala la Elimu katika watumiaji wa barabara pia tuliona haja ya kuongewa uwezo kwa watendaji wetu", DAUD DAUD- Katibu Mtendaji LATRA CCC.
Kwa kuzingatia hilo Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) wameingia Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa miaka mitatu na shirika la azaki za kiraia (FCS) ili kuimarisha ulinzi wa walaji na haki zao ndani ya sekta ya usafiri nchini Tanzania na hapa Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge anaelezea umuhimu wa mkataba huo
"Bila miundombinu ya usafiri iliyo imara inakuwa vigumu sana kwa taifa kufikia maendeleo na malengo yetu hatuwezi kuyafikia kama hatuna mifumo ya usafiri inayoeleweka kwahiyo huu ushirikiano wetu na baraza la ushauri ama watumiaji wa huduma za usafiri ni sehemu muhimu ya kuhakikisha miundombinu hii inaimarishwa inatumiwa vyema kwa manufaa ya kila mtanzania", JUSTICE RUTENGE-Mkurugenzi Mtendaji FCS
Baadhi ya wananchi wanatoa maoni yao ni sehemu gani inatakiwa maboresho.
"Tunatamani hizi barabara za mitaani ziongezwe ili kuboresha huduma za usafiri nchini kwa maana zikitumika zitapunguza adha ya msongamano kwenye barabara kubwa", HUSSEIN MPANDA-Mkazi wa Dar eś Salaam
"Tunashukuru Serikali imetujengea miundombinu bora sana lakini haijajali watembeaji wa miguu, tunaomba zinapojengwa barabara waweke na mitaro lakini izibwe ili watumiaji wa miguu na bodaboda waweze kupita bila changamoto", CHARLES GEORGE-Mkazi wa Dar es Salaam
"Kuna mitaro ipo kwenye barabara za mitaa na haijasafishwa kwahiyo inazalisha mazalia ya mbu kwahiyo wakati wanajenga wazingatie na njia ya kupita maji yanayoenda baharini ili kupunguza kero hiyo", SHEKH YUSUPH TONGE-Mkazi wa Dar es Salaam