Tuesday , 22nd Oct , 2024

Vikundi vya ulinzi shirikishi Kata ya Ngara Mjini wilaya ya Ngara mkoani Kagera vimetakiwa kuzingatia sheria kipindi cha utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kuwa mfano mzuri kwa jamii.

Vikundi vya ulinzi shirikishi

Hayo yamebainishwa na Mkaguzi Kata ya Ngara Mjini Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Olipa Chitongo wakati akitoa elimu kwa vikundi hivyo ambapo amewataka kufuata sheria za mwenendo wa makosa ya jinai akiwakumbusha kifungu cha 21 kifungu kidogo cha kwanza cha ukamataji salama.

Mkaguzi Olipa amewataka kutambua kuwa vikundi vya ulinzi shirikishi ni miongoni mwa wadau wa karibu wa Jeshi la Polisi katika masuala ya ulinzi ambapo amewasisitiza kufanya kazi kwa weledi ili kuzuia malalamiko na masononeko kwa wananchi.