Monday , 21st Oct , 2024

Msanii Marioo ameamua rasmi kuweka wazi kuwa ni kweli hayuko sawa na msanii mwenzie Chino Kidd ambaye amewahi kuwa chini yake kama dancer wake hapo nyuma.

Pichani ni Marioo Pamoja Na Chino Kidd

Kupitia Instagram story yake Marioo ameandika kuwa......"Ndugu zangu naomba mnisaidie kumuuliza Chino nini niliwahi kumkosea ambacho mimi sikijui zaidi ya sapoti, hili swala nimelikalia kimya muda mrefu sana lakini sasa naona limekuwa too much na mimi pia ni binadamu kila ninapo jitahidi kutengeneza mazingira ya amani na kukubali kuonekana fala ili kila mtu aishi maisha yake wananiona mimi mnyonge" Ameandika Marioo

"Hivi ni nani kamwambia Chino kuwa akitaka kuendelea kimuziki ni lazima anidharaulishe na aonekane ana matatizo na mimi? kama mnakumbuka alitoka kuniongelea vibaya sana kwenye mitandao mimi nikakaa kimya baadae akaja kuniomba msamaha nikamsamehe lakini nashangaa sasa hivi ameanza tena kuniongelea vibaya kwenye mitandao na kunidharaulisha."Ameandika Marioo

"Naombeni Mumuulize pengine yupo na sababu za msingi zinazo mpelekea yeye kutaka kunilipizia mimi ubaya pamoja na mazuri yote niliyowahi kumfanyia hapo nyuma,mpelekeeni hizo mic na camera zote awaeleze nini kibaya nilimfanyia'' Ameandika Marioo