Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amesema kuwa kati ya watu hao wanaume ni milioni 15,236,772 Sawa na 48.71% huku wanawake wakiwa milioni 16,045,559 Sawa na 51.29%
Hii ina maana kuwa Idadi ya Watanzania waliojitokeza kujiandikisha imeongezeka kwa 8%, ukilinganisha na uchaguzi wa mwisho wa mwaka 2019 ambapo watu waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la makazi walikuwa milioni 19 Kati ya watu milioni 22.9 waliokuwa kwenye umri wa kujiandikisha Sawa na 86%
Aidha Waziri Mchengerwa amewataka wananchi kuanza kuhakiki majina yao kwenye vituo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na zoezi hilo litadumu kwa siku saba
"Orodha ya wapiga kura kwenye kila kituo imeanza kubandikwa kuanzia leo ambapo wananchi wanaombwa kufika kwenye vituo walivyojiandikisha ili kuhakiki taarifa zao Kama kuna mahali zilikiwa zimekosewa na zoezi hilo litaenda kwa siku saba kuanzia leo Oktoba 21-27, 2024"