Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo
wakimbizi na kutafuta suluhisho la kudumu kulingana na maoni yatakayokusanywa katika mahojiano.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, alipowasilisha ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa 75 wa Kamati Tendaji ya UNHCR nchini Uswisi, tarehe 15 Oktoba 2024.
Mhe. Sillo amebainisha kwamba Tanzania inahifadhi wakimbizi zaidi ya 240,000, wengi wao wakiwa kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na serikali imefanikiwa kutafuta suluhisho la kudumu kwa wakimbizi 17,283 kwa mwaka huu, ambapo wakimbizi 12,717 walirudi kwa hiari katika nchi zao za asili, na 4,566 walipatiwa makazi mapya katika mataifa mengine.
Aidha Mhe. Sillo katika ujumbe wake alieleza kuwa licha ya mafanikio hayo, operesheni za kuhudumia wakimbizi nchini Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa za kifedha, hasa katika sekta za afya na elimu katika kutoa huduma bora kwa wakimbizi
Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa UNHCR, Filippo Grandi, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake katika kuhifadhi wakimbizi kwa miaka mingi na sasa kujikitika katika kutafuta suluhisho la kudumu kwa Wakimbizi hao. Aidha alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuungana ili kusaidia wahanga wa migogoro na kuhakikisha wanapata misaada inayohitajika