Mwanariadha wa Kenya mwenye umri wa miaka 30 Ruth Chepngetich ameweka rekodi mpya Chicago Marathon alitumia masaa mawili na dakika 9 na sekunde 57 na kuvunja rekodi iliyowekwa na Assefa mwaka 2023 ambaye alikimbia mbio ndefu kwa masaa mawili dakika 53 na sekunde 53. Chepngetich pia amewahi kushinda ubingwa wa Dunia mwaka 2019.
Mwanariadha wa Kenya anayekimbia mbio ndefu Ruth Chepngetich ameweka rekodi mpya siku ya jana Oktoba 13 nchini Marekani baaada ya kukimbia mbio ndefu za Chicago ( Chicago Marathon ) kwa kutumia masaa mawali dakika 9 na sekunde 57.
Mkimbiaji huyo amevunja rekodi iliyokua unashikiliwa na Assefa aliyekimbia mbio ndefu kwa masaa mawili dakika 11 na sekunde 53. Chepngetich anakuwa Mwanamke wa kwanza kukimbia mbio ndefu kwa kutumia masaa mawili na chini ya dakika 10.
Chepngetich mwenye miaka 30 ameshainda mbio ndefu za Chicago kwa sasa anatizamwa kama Mwanariadha wa kike anayefanya vizuri zaidi katika Ulimwengu wa riadha Duniani. Wanariadha wa Kenya Wanarekodi nzuri kwenye mbio ndefu wameshinda mataji ya mbio ndefu kwa kuvunja rekodi mbalimbali.
Mkenya John Korir ameweka rekodi kwa upande wa Wanaume baada ya kukimbia kwa masaa mawili dakika 2 na sekunde 44. Katika tano bora za Mbio ndefu za Chicago Wanne ni Wanariadha kutokea Kenya na Mmoja raia wa Ethipoia.
Ushindi wa Ruth Cheongetich ulikuwa maalumu kwa kumkumbuka Kelvin Kiptum aliyetwaa ubngwa wa Mbio ndefu za Chicago mwaka jana na baadae kufariki kwa ajali ya gari, Kiptum alifariki akiwa na miaka 24.
Bingwa huyo wa Mbio ndefu za Chicago kwa upande wa Wanawake amejitengenezea utawala wake katika mashindano hayo ndani ya miaka minne ameshinda ubingwa mara tatu mwaka 2021, 2023 na 2024 sambamba na ubingwa wa Dunia mwaka 2019.