Dkt. Chana ameyasema hayo katika tamasha la utamaduni jamii za watu wa kigoma ambalo limefanyika hii leo ambapo amesema vikundi vidogo vinaweza kukodishwa kwenda kutumbuiza sehemu mbalimbali na kujiingizia kipato na kukumbusha jamii tamaduni zao
“Licha ya urithi wa utamaduni kutumika kwa shuguli za elimu, burudani, utafiti pia urithi huu umekuwa unaendeleza uhusiano na heshima miongoni mwa watu wa mataifa kwa vipindi vyote vya historia ya jamii mbalimbali wananchi wanaweza wakatumia tamaduni kama chanzo cha mapato hivyo kujipatia ajira na kuboresha hali za maisha, zamani tulikuwa tunafanya utamaduni kwa kujiburudisha lakini hizi ngoma mnaweza mkaunda kikundi, kikundi hicho kikawa ni ajira watu wanaweza kukodi ngoma waende wakatumbuize sehemu Fulani, lakini pia tunayo mikopo kwa ajili ya wasani na katika almashauri zetu tumetenga pesa kwa ajili yenu” Amesema Dkt. Pindi Chana.