Tuesday , 8th Oct , 2024

Katibu mkuu chama cha mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewapokea wanachama Zaidi ya 60 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kuhamia CCM katika wilaya ya Itirima mkoani simiyu

Katibu mkuu CCM Balozi Dkt. Nchimbi akiwakaribisha wanachama wapya mkoani simiyu

Mapokezi hayo yamefanyika wakati Dkt. Nchimbi akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu ambapo mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Itirima na wafuasi wake wamehamia CCM ambapo Dkt. Nchimbi amesema wanachama wamehamia CCM kwa kuona kazi nzuri inayofanywa na Viongozi wa chama hicho,

“Ndugu zetu kutoka upinzani, Zaidi ya 60 wamejiunga na CCM leo na wamejiunga baada ya kushawishika na kazi nzuri za maendeleo zilizofanyika lakini pia wamefarijika na kazi zinazofanywa na mbunge wenu” Amesema Dkt. Nchimbi