Monday , 30th Sep , 2024

Wanawake walio katika umri wa miaka 30-40, wametakiwa kupima Afya zao mara kwa mara ili kama kuna tatizo kwenye mifumo yao ya uzazi iweze kutibiwa kwa haraka kuliko kusubiri tatizo kuwa kubwa na kusababisha madhara na gharama kubwa za matibabu.

Dkt.Abdallah Mashombo, Daktari Bingwa magonjwa ya wanawake TRRH.

Daktari wa madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, Dokta Abdallah Mashombo, wakati anaongea na EATV, kuhusu  magonjwa ya wanawake ambayo yamekuwa yakigundulika yamekomaa.
"Ushauri wangu ni vema wanawake walio katika umri wa reproductive kucheck afya zao mara kwa mara ili waweze kujua Afya zao mapema na baada ya kujua watafanya matibabu ya haraka kwa sababu wao ndio wapo katika umri wa uzalishaji na magonjwa ya uvimbe hayana dalili ndio maana wengi huwa wanakuja kugundua tatizo limeshakuwa kubwa kitu ambacho kinaweza kutibika mapema", alisema Dkt.Abdallah Mashombo, Daktari Bingwa magonjwa ya wanawake TRRH.

Aidha anaelezea sababu za wanawake kupata changamoto hizo.
"Miongoni mwa sababu ya hizo vimbe ni mabadiliko ya kiomoni, kubwa sana hizi vimbe hazina sababu yeyote labda ni maambukizi kutoka sehemu nyingine hapana bali ni zile mbegu za kike zikishindwa kujiregulatre zinawezaq kusababisha vimbe", alisema Dkt.Abdallah Mashombo, Daktari Bingwa magonjwa ya wanawake TRRH.

Hospitali ya Mkoa ya Rufaa ya Temeke, juma lililoisha lilifanikiwa kufanya upasuaji kwa mwanamke wa umri wa miaka 51 na kufanikiwa kutoa uvimbe wa kilogram 6.4 alioishi nao kwa muida wa miaka 16.
Wananchi wengi wamekuwa wazito kufika hospitali kuangalia Afya zao bila ya kuumwa, hali ikoje kwa baadhi ya wanawake waishio Temeke.
"Mimi huwa napima Afya yangu kila baada ya miezi sita na namshukuru Mungu kwa nyakati nilizoenda sijawahi kukutwa na changamoto yeyote", alisema Yasista Mbise, Mkazi wa Temeke.

"Mimi huwa naenda endapo nina dalili ya kuumwa sijawahi kutoka nyumbani nikaenda Hospitali kupima kama siumwi, siku moja nilitoka nikaebnda nikakutwa nab UTI, nikatibu mpaka leo sina tatizo lolote", alisema Joyce Petro, Mkazi wa Temeke.

"Naishauri Serikali iongeze elimu ya umuhimu wa kupima afya zetu kabla ya kuumwa hii itasaidia kupata matibabu ya haraka kuliko kuubiri ugnjwa kukomaa", alisema  Swaum Miraji, Mkazi wa Temeke.