Friday , 20th Sep , 2024

Watanzania na wadau mbalimbali wamepewa wito kwa ajili ya kufanikisha ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 100 wa kitanzania waliokwama kuendelea na masomo ya Elimu ya kutokana na changamoto ya kiuchumi.

Wito huo umetolewa na mratibu wa mbio za Mbuzi kutoka Rotery Club ya Oysterbay, Paul Muhato huku akielezea namna mbio hizo zitakavyonufaisha wanafunzi wa kitanzania.
"Mbio hizi zimelenga kusaidia kupunguza ya Elimu kwa vijana wa kitanzania ambao walisoma lakini wakashindwa kuendelea na Elimu ya juu kutokana na changamoto ya kifedha, hatutaishia kwenye ufadhili wa masomo peke yake lakini pia kupunguza changamoto za miundombinu ya Elimu nchini", alisema  Paul Muhato, Mratibu mbio za Mbuzi.

Aidha mratibu anaelezea namna mbio hizi zitakavyofanyika.
"Tutashindanisha Mbuzi ambao watakuwa kwenye makundi nane na atakayeshinda atapata zawadi, na kwenye mbio hizi kiasi kitakachopatikana kitanenda kupunguza changamoto ya miundombinu ya Elimu nchi tnawakaribisha wananchi kujitokea kwa wingi kushiriki", alisema Paul Muhato-Mratibu mbio za Mbuzi.

Kwa wale ambao hawajui wanawezaje kushiriki mbio hizi, mratibu anatolea ufafanuzi.
" kiingilio cha kawaida kwa wakubwa ni shilingi 30,000/=, na watoto 10,000/=, kwa upande wa wageni maalum wakubwa ni shilingi 220,000/= na watoto ni shilingi 30,000/=",  alisema Paul Muhato, Mratibu mbio za Mbuzi.