Shekhe Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na amani Tanzania.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na amani Tanzania, Shekhe Alhad Mussa Salum,akiongea na wanahabari leo akisema kuwa kuna haja ya viongozi wa mitaa kupewa Elimu kuhusu kuzuia matukio.
"Matukio haya yanatokea kwenye jamii zetu kwahiyo hawa viongozi wa chini wakielimishwa namna ya kukabiliana na watu wapya kwenye jamii yao inayowazunguka na kutoa ushirikiano kwa Jeshi ili kusaidia kuwapata watekelezaji wa matukio hayo" alisema Shekhe Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na amani Tanzania.
Aidha viongozi wa Dini wamekusudia kuliombea Taifa kwa ajili ya kupunguza vitendo vya ukatili ambavyo vinaendelea nchini kwetu ifikapo Septemba 21, 2024.
"Tumepanga kufanya maombi kwa ajili ya kuliombea Taifa ili tuweze kuondokana na mauaji haya ambayo kwa sasa yamekithiri kila kona kwenye nchi yetu na yatafanyika Septemba 21, 2024 kwenye viwanja vya karimjee jijini Dar es Salaam na mgeni Rasmi atakuwa makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt.Philip Mpango",alisema Shekhe Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na amani Tanzania.
Nao baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam, wanaelezea kwanini hivi vitendo bado vinaendelea kwenye jamii yetu.
"Vijana mtaani wanabaka, wanalawiti lakini wakikamatwa wanaachiliwa inamaanaa hivi vitendo vitakuwa vinaenelea kwenye jamii yetu, inabidi Serikali na Jeshi la Polisi kuongeza doria za mara kwa mara ili kupunguza vitedno hivi", alisema Cassmir Marandu, Mkazi wa Dar es Salaam.
"Vijana wengi hawana ajira lakini kama wangekuwa nazo ina maana wangekuwa busy kufanya kazi na sio kuwaza kufanya ukatili pia vyombo vya Sheria vitende haki na hao watu waadhibiwe ili kuonesha kuwa ni kosa", alisema Rahim Zahoro, Mkazi wa Dar es Salaam.