Tuesday , 17th Sep , 2024

Muigizaji,rapa na mfanyabiashara 50 Cent amemtaja Kendrick Lamar kustahili kuperforme Super Bowl Halftime show pande za New Orleans anapotokea Lil Wayne.

Kutoka kushoto ni 50 Cent, Kendrick Lamar na Lil Wayne

50 Cent anasema ku-performe Super Bowl ni chaguo na msanii Solo anayestahili kwa sasa ni Kendrick Lamar.

Ikumbukwe 50 Cent alishiriki kufanya show hiyo ya Super Bowl mwaka 2022 baada ya kualikwa na Dr. Dre na kushea stage moja na wasanii kama Kendrick Lamar, Snoop Dogg, Eminem, Mary J. Blige na Anderson Paak.