Prof. Andrew Swai, Mwenyekitu Chama cha watu wenye Kisukari.
Wito huo umetolewa na meneja mradi wa shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Happy Nchimbi akiongea na EATV kuhusu namna ya kujiminga na magonjwa hayo.
“Magonjwa haya sio ya kurogwa bali ni mtindo wa maisha , ulaji na matumizi ya Sukari, Chumvi, Pombe na Tumbaku, kwa sababu inaweza kukuletea ugonjwa wa Sukari, Figo, Moyo na magonjwa yote yana gharama kuyatibu”, Happy Nchimbi, Meneja Mradi (TANCDA).
“Jamii inahita Elimu sahihi ya kujikinga, kuangalia mtindo wao wa maisha, kukabiliana na tatizo na namna ya kuepuka tatizo, jamii ikifanikiwa kupata elimu sahihi tuna amini itajitahidi kukabiliana na kagonjwa haya ambayo kwa sasa yanachangia vifo kwa kiasi kikubwa ma Serikali inatumia gharama nyingi kuyatibu”, alisema Dkt.Anna Nswilla, Mshauri chama cha Magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Kisukari Profesa Andrew Swai anatoa kanuni nane za mfumo bora wa maisha.
“Kila mlo uwe na aina zote za vyakula, Usivichakachue vyakula, Usile kwa wingi, Jishughulishe nchana, Pumzika usiku, Usitamani ya watu, Epuka tumbaku, Chunguza Afya kila mwaka”, alisema Prof. Andrew Swai, Mwenyekitu Chama cha watu wenye Kisukari.
Nao waandishi na wasanii wanaelezea jukumu lao katika kutoa Elimu ya namna bora ya kujikinga na magonjwa hayo.
"Waandishi tunatakiwa tutumie kalamu zetu katika kuandaa vipindi, kutengeneza habari ambazo zitaelezea ukubwa wa changamoto na namna ya kutatua chanagmoto hii kwa usahihi", alisema Sophia Mganya, Meneja Utangazaji EATV.
“Magonjwa haya yapo na yanatisha mimi kama msanii kama ambavyo tulitoa Elimu kwenye Ugonjwa wa Ukimwi, nitatumia platform zangu kutoa Elimu juu ya magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza ili kusaidia jamii kuepukana nayo”, Mwasiti Almas, Msanii wa Bongo Fleva.
“30% ya vifo nchini vinatokana magonjwa yasiyo ya kuambukiza mimi kama mwanahabari nitatoa Elimu ya kutosha na kuandika kwa usahihi namna ya kujikinga na kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ili kuweza kuisaidia jamii yetu”, Kissa Daniel, Mwandishi wa Habari EATV.