Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu
Ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha wakati akizungumza na wataalam kutoka kwenye taasisi mbalimbali za serikali ambao wamechaguliwa kuwa wanajopo wa kuendesha zoezi la usaili wa mahojiano ya ana kwa ana kwa wasailiwa kada ya afya unaendelea katika mikoa mbalimbali nchini.
Amesema serikali imejipanga kuhakikisha haki inatendeka kwa kila msailiwa ili atakayeshinda ashinde kwa haki na atakayeshindwa ashindwe kwa haki.
Mhe. Sangu ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wanajopo hao kutanguliza mbele maslahi ya taifa huku akionya yeyote atakayethubutu kuvuruga zoezi hilo atakuwa ameingia kwenye matatizo makubwa
"Tunatafuta vijana watakaoingia serikalini katika utumishi wa umma si chini ya miaka 25 na wengine wenye umri mdogo mpaka miaka 30 kwahiyo tukifanya makosa tukapeleka vijana wasio na sifa, uadilifu na mengineyo tutalighalimu taifa kwa zaidi ya miaka 25," amesema