Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumanne Agosti 27, 2024, na Msemaji wake, David Misime, Zakia amekiri kumuiba mtoto huyo na anaendelea kushikiliwa ili kukamilisha uchunguzi.
"Imebainika kilichomfanya kufanya tukio hilo ni baada ya kupata taarifa ya mtu aliyekuwa anatafuta mtoto asiye na wazazi na anaishi katika mazingira magumu ili aweze kufuata taratibu za kumwasili, kutokana na tamaa zake yeye akaona ni dili amepata na akisukumwa na tamaa hizo akaenda kuiba mtoto huyo," imeeleza taarifa ya polisi
Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Alipoambiwa waanze kufuata taratibu na kutakiwa alete wanandugu wengine, vyeti na waende kwa kiongozi wa serikali za mitaa kwa utambuzi alianza kusita na kushindwa kutekeleza masharti hayo, ndipo mashaka yakaanza na kupelekea kumtilia shaka mashaka mengine yalijitokeza pale alipoanza kudai ajengewe nyumba ya vyumba vitatu au apewe milioni 50,"