Gawio
Dkt. Biteko amepokea gawio leo Agosti 26, 2024 jijini Dar es Salaam huku akishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa nchi hizo mbili ambapo ni miaka mitano tangu kutolewa kwa gawio mwaka 2019.
Amesema mapokezi ya gawio hilo ni matokeo ya ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan nchini Zambia ambapo alielekeza miradi isimamiwe vizuri ili ilete matunda na kubadili maisha ya watu wa nchi hizo mbili
"Nawapongeza sana Bodi ya TAZAMA na Wizara ya Nishati kwa hatua hii, haya ni matokeo ya ziara ya Mheshimiwa Rais nchini Zambia ambapo alituelekeza miradi hii tuisimamie na ilete matunda na kubadili maisha ya watu wa nchi zetu." Amesema Biteko
Aidha, ameitaka TAZAMA kuendelea kulisimamia vizuri Bomba hilo ili lizidi kuleta faida ambapo mikakati iliyopo sasa ni kuongeza ukubwa wa bomba la TAZAMA kutoka inchi nane hadi inchi 12.