Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania, Awadhi Juma Haji
Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania, Awadhi Juma Haji ambaye amesema jeshi la polisi litaendelea kupambana na viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani ikiwemo maandamano hayo ambayo yamelenga kuvuruga amani
Amewaagiza makamanda wa Polisi wa Mikoa (RPC) kufanya ukaguzi kwenye mabasi yanayoelekea jijini Mbeya kwenye kongamano la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuwachukua hatua wahusika.
Haji ametoa maagizo hayo leo Jumapili, Agosti 11, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya ikiwa kufuatia uwepo wa taarifa za kongamano hilo lililopangwa kufanyika kesho Jumatatu, Agosti 12, 2024, Viwanja vya Ruanda Nzomve kupigwa marufuku na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.