Kwa mara ya kwanza ameonesha kuwa upande wa chama chake, kwa kuungana na wanachama wa Democratic kumpa nguvu Kamala Harris ambaye anatarajiwa kusimama kama mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama Democratic huku mpinzani wake mkubwa ni Rais wa zamani wa taifa hilo na mwanachama wa chama cha Republican Bw, Donald John Trump
Haya yanajiri baada ya makamu wake wa zamani Joe Biden kutangaza kutogombea kwa muhula ujao, kutokana na changamoto binafsi ikiwemo kiafya
Kupitia mitandao yake ya kijamii Obama ameandika; Mapema wiki hii, mimi na Michelle (ambaye ni mke wake) tulimpigia simu rafiki yetu Kamala Harris na kumwambia kuwa anaweza kuwa Rais mzuri wa taifa la Marekani, tunamuunga mkono na kumpa ushirikiano kwenye wakati huu muhimu kwenye taifa letu, tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha anashinda kwenye uchaguzi wa Novemba, yetu matumaini ni kwamba utaungana nasi.