Rais wa Kenya William Ruto
Rais Ruto ametangaza Baraza hilo hii leo Julai 24, 2024, ambapo miongoni mwa wapinzani aliowateua ni Hassan Joho kuwa Waziri wa Madini na John Mbadi akiteuliwa kuwa Waziri wa Fedha, zikiwa zimepita siku tano tangu litangazwe lile la awali na kuwarudisha sita waliokuwa mawaziri katika baraza alilolivunja.
Hatua hiyo imekuja kufuatia maandamano ya vijana nchini humo ambao wamekuwa wakipinga ugumu wa maisha na ongezeko la kodi pamoja na kumtaka Rais Ruto kung'oka madarakani.
Hawa ndiyo mawaziri walioteuliwa hii leo, Salim Mvurya kuwa Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Rebecca Miano Waziri wa Utalii, James Wandayi Waziri wa Nishati, Kipchumba Murkomen Waziri wa Michezo, Hassan Joho Waziri wa Madini, Alfred Mutua Waziri wa Kazi, Wycliffe Oparanya Maendeleo ya Ushirika wa Biashara zinazochipukia na za Kati, Justin Muturi Utumishi wa Umma na Stella Soi Lang’at akishughulikia Masuala ya Jinsia huku John Mbadi akiteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.