Sunday , 14th Jul , 2024

Pale Kenya Khaligraph Jones anasema ‘Respect the OG’ wazungu wao ‘Legend Never Die’ na #MwanaFA anakwambia ‘Keep The Good Music Alive’ misemo yote hiyo inawatafsiri watoto wa Mzee Okoye 'Paul & Peter' P Square kwenye Muziki.

Picha ya P Square

Nyota yao ya muziki ilianza mwanzoni mwa miaka ya 2000 na kuachia mfululu wa Hits back to back kama Do Me, Ifunanya, No one like you, Temptation, Beautiful Onyine, Personally, Alingo, Taste The Money, Chop my money, Forever, Collabo, Bring it on, Bizzy Body, No Easy na Testimony.

P SQUARE ni zaidi ya wasanii wana vipaji na uwezo mkubwa wa kuandika, kuimba, ku-perfome live, kucheza, ku-entertain, ku-inspire na Legacy waliyoitengeneza kwenye muziki wa Africa.

Hizi International Collabo zinazofanywa na wasanii wa sasa wa Africa Magharibi P Square walishafanya kitambo kama Rick Ross na TI tena wakiwa wamoto kwelikweli pia ni wasanii wa kwanza muziki wao kutambulika zaidi soko la kimataifa.

Wanatajwa kama wasanii wenye ushawishi zaidi Africa, Kundi bora la muziki liliofanikiwa zaidi katika Karne ya 21 Africa, wasanii bora wa Muongo mmoja kupitia tuzo ya MTV Africa Music Awards 2015 na Forbes wanawataja kama wasanii wenye nguvu zaidi Africa.

Kwenye hao 'GOAT African Artist' usiwasahau P Square, achana na watoto wa 2000 ambao wamekua wakiwaona Burna Boy,Davido,Rema na Wizkid wanafanya vizuri na kuvunja rekodi kila siku.