Monday , 24th Jun , 2024

YouTube imejichukulia sheria mkononi kwa mara ya kwanza mara baada ya watumiaji wa huduma ya YouTube Premium kushindwa kutambua mipaka yao.

 

Kupitia mtandao wa Reddit watumiaji baadhi wa huduma ya Premium inayotolewa na mtandao wa YouTube wameonekana kukasirishwa na kulalamika, na hii nikutokana na vifurishi vyao kufutwa kwenye mtandao wa YouTube.

Haya yanajiri baada ya watumiaji wa huduma ya Premium waliotumia njia ya VPN kwenye ununuaji wa vifurushi kwenye mtandao wa YouTube ili kupata punguzo, kushtukiwa na YouTube wenyewe.

Ilivyo, Baadhi ya watumiaji wa huduma ya Premium walitumia VPN kwenye kulipia huduma hiyo ili kudanganya maeneo yao halisi na kupata punguzo kwenye ulipaji wa huduma hiyo mfano mtumiaji wa huduma ya YouTube premium wa nchini Argentina alihitajika kulipa kiasi cha 2,761 pekee kwa mwezi, lakini mtumiaji wa huduma hiyo hiyo kutokea nchini Marekani alihitajika kulipia kiasi cha 36,793 kwa pesa ya Tanzania kwa huduma ya Premium kwa mwezi.

Umuhimu wa YouTube Premium, Unaweza kuwa unajiuliza kwa nini watu wanalipia huduma hii hapa nitakupa faida tatu tu, Moja ni kuepuka matangazo ukitumia huduma hii hupati matangazo Pili ni kuwezeshwa kupakua video hata kama huna bando offline downloads Tatu kupata huduma ya YouTube Music ambayo inakupa huduma ya muziki kwa ukubwa zaidi kama Spotify fulani hivi.