Thursday , 20th Jun , 2024

Msafara wa timu ya Tanzania kwa mchezo wa Kuogelea unataraji kuondoka kesho Ijumaa Juni 21-2024 kuelekea nchini Kenya kushiriki shindano la Taifa kwa umbali mrefu linalotaraji kufanyika kuanzia Juni 23-2024.

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi bendera Waogeleaji hao,Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Abel Odena amewataka wachezaji hao kwenda kupambana ili kuhakikisha wanarudi na medali nyumbani kutoka kwenye shindano hilo.

"Nendeni mkapambane kuhakikisha mnakwenda kuipeperusha vema bendera ya Taifa kwa kupata medali nyingi za dhahabu kwani kila kitu kinawezekana, amesema  Odena.

Kwa upande wake,Kocha Mkuu wa timu ya Kuogelea ya  Tanzania Alexander Mwaipasi amesema  shindano hilo la Taifa la Kuogelea la Kenya wanakwenda kama timu waalikwa huku timu hiyo itawakilishwa na wachezaji 4 pekee kwenye shindano hilo.