Thursday , 20th Jun , 2024

Kama ulidhani kuwa talanta ya uchekeshaji ya mchekeshaji maarufu Tanzania kwa sasa, Leonardo imeanza ukubwani basi habari mpya ni kwamba Leonardo hivi karibuni amedokeza kuwa tangu akiwa mwanafunzi shuleni, alikuwa ni mchekeshaji mzuri tu.

 

Leonardo ambaye hivi karibuni alipamba vichwa vya habari Tanzania baada ya kujaza ukumbi wa Mlimani City akiwa na mchekeshaji mwenzake Ndaro kwenye show kubwa ya kihistoria amedokeza kuwa alianza kuchekesha tangu akiwa mwanafunzi.

 

Wakati nakua nilikuwa kituko. Nilikuwa ni moja ya wale ma-backbencher ambao mwalimu akiwa amechapia basi nitaonesha kuwa amechapia na darasa zima litacheka.

 

Na hata muonekano wangu pia ulichangia kuonekana kituko. Nilikuwa mwembamba afu nina masikio makubwa. Lakini uzuri pia nilikuwa na akili darasani kwa hiyo haikua ishu kubwa na kulikuwa na heshima kidogo.

 

 

Leonardo pia alidokeza kuwa alisoma Shule ya msingi Kilakala na elimu ya Sekondari aliipata Shule ya Sekondari Morogoro na baadae alihamia Galanosi High School kumalizia elimu ya Form 6 kisha akachaguliwa kwenda kwenye Chuo Cha Maji Dar Es Salaam kwa ajili ya kupata shahada yake ya kwanza.

 

Ikumbukwe kuwa Leonardo alianza tasnia ya uchekeshaji mwaka 2019 alipojiunga na  kampuni ya Punchline Comedy Club ya Evans Bukuku na mwaka 2021 alijiunga rasmi na Cheka Tu baada ya kushinda mchuano wa Cheka Tu Comedy Search ambapo aliondoka na kitita cha Tsh Milioni 10.