Wednesday , 5th Jun , 2024

Kufuatia matukio mbalimbali yanayohusisha ukatili wanaofanyiwa watu wenye Ualbino nchini, Chama cha watu wenye ulemavu (TAS) kimeomba kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuzungumza nae kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye Ualbino Tanzania.

Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania TAS, Godson Molle

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ualbino Tanzania TAS, GODSON MOLLE ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu tukio la kuporwa kwa mtoto mwenye Ualbino kufanyika huko Muleba mkoani Kagera 

Leo Kupitia vyombo vya habari ikiwemo EATV amesema kama chama cha watu wenye Ualbino wanalaani vikali matukio haya ya kikatili wanaofanyiwa watu wenye Ualbino ambapo amewasilisha ombi hili kwa serikali na viongozi wengine wenye Mamalaka Nchini kuibuka na kukemea matukio kama haya 

Mbali na ombi hilo amesema kila mwenye madaraka, nafasi katika muhimili wowote wa Nchi ikiwemo Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania watoe matamko kuhusu vitendo hivi na kuangalia namna mtoto huyo anaweza kupatikana 

"Sisi ni wananchi kama wananchi wengine tunawabunge wetu waliopo bungeni ambao tumewachagua watuwakilishe tunaomba na wao waseme neno sio kukaa kimya na sisi tunahaki ya kuishi bila kugudhiwa kwa amani na utulivu kwasababu hatuna amani sasa", GODSON MOLLE - Mwenyekiti chama cha watu wenye Ualbino Tanzania