Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Saturday , 27th Apr , 2024

Katika kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na afya mahali pa kazi namna ya kuzingatia usalama wawapo katika shughuli zao, Kampuni ya Geita Gold Mining Ltd (GGML) imeleta vifaa mbalimbali vya kisasa ili kutoa fursa kwa washiriki kujifunza teknolojia za kisasa za uokoaji.

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

Hayo yamebainishwa na Meneja Usalama kutoka GGML, Isack Senya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho hayo yanayofanyikakwenye viwanja vya General Tyre jijini Arusha na kuratibiwa na wakala wa usalama na afya mahali pa kazi (OSHA).

“Kama kawaida GGML kwa kutambua umuhimu wa afya na usalama kazini na ikiwa ni tunu yetu ya kwanza, GGML ina wawakilishi zaidi ya 45 kwenye maonesho haya wanaotoa elimu mbalimbali kuhusu masuala ya afya na usalama kazini,” alisema Senya.

Senya alisema katika maonesho hayo wamekuja na vifaa mbalimbali ikiwamo rada maalumu ambayo ina uwezo wa kutambua ukuta ambao una udhaifu au unaoweza kuanguka pindi shughuli za uchimbaji mgodini zikiendelea.

Alisema rada hiyo hutoa ripoti mapema ili kuondoa watu kwenye maeneo husika iwapo ukuta au mwamba huo unataka kuanguka.

“Kifaa hiki kinaangalia eneo la uchimbaji na kinavyozunguka kinapiga picha za satellite. Picha hizi zinarejeshwa kwenye mfumo na kuona kama kuna mwenendo wowote wa ukuta unaoweza kuleta athari, inamtahadharisha mtalaamu na kuchukua hatua stahiki. 

“Rada hii ilisaidia sana mwaka 2007 ambapo kulitokea maporomoko makubwa sana ya ukuta lakini kutokana na kifaa hiki, yalibainika mapema na kuchukua hatua stahiki ikiwamo kudhibitiwa,” alisema.

Alisema pia timu ya GGML imekuja na mambo mengi zaidi na tofauti kulingana na kaulimbiu ya mwaka huu inayosema “mabadiliko ya tabia nchi na athari usalama na mazingira.”

“Tumeona madhara mbalimbali yaliyotokana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo tumeona ni muhimu sasa kuhakikisha elimu zetu tunazotoa zinajikita kwenye maeneo hayo,” alisema na kuongeza pia katika banda hilo wanatoa huduma za awali za afya ikiwamo upimaji wa magonjwa ya kisukari na presha.

Mbali na rada pia alisema GGML wameleta boti ya uokoaji majini, vifaa vya uokoaji katika uchimbaji chini ya ardhi pamoja na kutoa elimu kuhusu majanga makubwa na vidhibiti majanga ambayo yanaweza kuepukwa.

Alisema katika maonesho hayo tayari wameshatoa mafunzo ya namna ya kujikinga na kukabiliana na majanga ya moto kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha pamoja na kuwagawia mitungi ya gesi ya kupikia.

Pia alisema wanatarajia kutoa mafunzo kwa madereva pikipiki kuwaelimisha namna ya kuzingatia usalama pindi wawapo katika shughuli zao. 

Alisema kutokana na mifumo imara ya udhibiti majanga pamoja na kuzingatia masuala ya afya na usalama kazini kwa muda wa zaidi ya miaka 14 sasa ndani ya GGML hakuna kifo kilichotokea kutokaa na shughuli hizo za uchimbaji.
 

HABARI ZAIDI

Rais wa Iran Ebrahim Raisi

Rais wa Iran afariki kwa ajali ya Helikopta

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,

China yaahidi kuendelea kufadhili miradi Tanzania

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12