Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha Benchikha amesema kuna tofauti kubwa ya Al Ahly aliyokutana nayo dhidi ya USM Alger huku kwa upande wa kikosi cha SImba wamejiandaa vyema kusaka ushindi kwenye mchezo wa kesho.
“Matokeo ya nyuma ni mengine, timu iliyopo sasa tofauti ya awali, Matokeo ya kesho ndio yataamua, kila mmoja anatambua ukubwa wa Al Ahly, siwezi kutabiri lakini tumejipanga kwa ajili kwa ajili ya kusaka ushindi’’amesema Benchikha.
Kwa upande wa Kocha Al Ahly, Marcel Koller amesema haitakuwa mechi rahisi kwa sababu wanakutana na timu waliyokutana katika michezo ya African Football League (AFL) mara mbili na zote kutoka sare katika michezo yote.
“Nimecheza nao mechi mbili na zote nimetoka nao sare, iliwaona na naweza kusema kuwa wapo kwenye level kama yetu na wala sio timu ndogo. Tunawaheshimu na kucheza kwa umakini mkubwa’’amesema Marcel.